Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 49
Bible en Swahili de l’est


1 Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. Nombres 24.14 Daniel 10.14 Jérémie 23.20 Deutéronome 4.30 Apocalypse 4.1
2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu. Psaumes 34.11 Proverbes 7.24 Proverbes 6.20 Proverbes 23.22 Proverbes 23.26
3 Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Deutéronome 21.17 Psaumes 78.51 Genèse 29.32 Psaumes 105.36 Nombres 26.5
4 Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu. Genèse 35.22 1 Chroniques 5.1 Deutéronome 27.20 Jacques 1.6-1.8 2 Pierre 2.14
5 Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri. Genèse 34.25-34.31 Genèse 29.33-29.34 Proverbes 18.9 Genèse 46.10-46.11
6 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng’ombe; Psaumes 26.9 Genèse 34.30 Psaumes 64.2 Psaumes 57.8 Psaumes 16.9
7 Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli. Josué 19.1-19.9 1 Chroniques 4.24-4.31 Proverbes 26.24-26.25 2 Samuel 13.22-13.28 1 Chroniques 6.65
8 Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. 1 Chroniques 5.2 Genèse 27.29 Hébreux 7.14 Deutéronome 33.7 Genèse 29.35
9 Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha? Nombres 24.9 Nombres 23.24 Michée 5.8 Apocalypse 5.5 Osée 5.14
10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. Psaumes 60.7 Nombres 24.17 Luc 1.32-1.33 Esaïe 42.1 Jérémie 23.5-23.6
11 Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu. 2 Rois 18.32 Michée 4.4 1 Rois 4.20 Apocalypse 7.14 Apocalypse 19.18
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa. 13 Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni. Deutéronome 33.18-33.19 Genèse 30.20 Josué 19.10-19.16
14 Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo; 1 Chroniques 12.32 Genèse 30.18 Josué 19.17-19.23 Juges 5.15-5.16 Deutéronome 33.18
15 Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu. Psaumes 81.6 Josué 14.15 Matthieu 23.4 Ezéchiel 29.18 2 Samuel 7.1
16 Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya Israeli; Deutéronome 33.22 Genèse 30.6 Juges 13.2 Juges 18.1-18.2 Juges 13.24-13.25
17 Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali. 1 Chroniques 12.35 Juges 14.1-14.15 Juges 18.22-18.31 Juges 16.22-16.30
18 Wokovu wako nimeungoja, Ee Bwana. Psaumes 119.166 Psaumes 119.174 Esaïe 25.9 Michée 7.7 Luc 2.25
19 Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino. Genèse 30.11 Juges 10.1-10.11 Josué 13.8 Genèse 46.16 Deutéronome 33.20-33.21
20 Asheri, chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalme. Deutéronome 33.24-33.25 Genèse 30.13 Genèse 46.17 Josué 19.24-19.31
21 Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri. Deutéronome 33.23 Genèse 30.8 Juges 4.10 Psaumes 18.33-18.34 Juges 4.6
22 Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matwi yake yametanda ukutani. Genèse 41.52 Genèse 48.19-48.20 Psaumes 1.1-1.3 Genèse 48.5 Josué 17.14-17.17
23 Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi, Genèse 37.24 Genèse 37.28 Psaumes 64.3 Jean 16.33 Genèse 42.21
24 Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli, Psaumes 132.2 Esaïe 28.16 Psaumes 132.5 Psaumes 18.30 Job 29.20
25 Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba. Genèse 28.13 Genèse 35.11 Genèse 35.3 Philippiens 4.19 Genèse 17.1
26 Mibaraka ya baba yako Imepita mibaraka ya milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake. Deutéronome 33.15-33.16 Habakuk 3.6 Genèse 37.28 Psaumes 105.17-105.22 Psaumes 132.18
27 Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-rarua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka. Juges 20.21 Genèse 35.18 Ezéchiel 22.27 Juges 20.25 Jérémie 5.6
28 Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake aliwabariki. Ezéchiel 39.8-39.10 Esther 8.11 Esther 9.1-9.10 Apocalypse 7.4 Genèse 35.22
29 Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti; Genèse 50.13 Genèse 47.30 Genèse 15.15 Genèse 35.29 Romains 12.6-12.21
30 katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia. Genèse 23.8-23.9 Genèse 23.16-23.18 Genèse 23.20
31 Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea; Genèse 35.29 Genèse 25.9 Genèse 23.3 Genèse 23.16-23.20 Genèse 50.13
32 shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi. Genèse 23.17-23.20
33 Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake. Genèse 49.29 Genèse 25.8 Josué 24.27-24.29 Esaïe 57.1-57.2 Genèse 35.29

Cette Bible est dans le domaine public.