Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Michée 3
Bible en Swahili de l’est


1 Nikasema, Tafadhali sikieni, enyi vichwa vya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli. Je! Haiwapasi ninyi kujua hukumu? Jérémie 5.4-5.5 Esaïe 1.10 Osée 5.1 Psaumes 82.1-82.5 1 Corinthiens 6.5
2 Ninyi mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na nyama mifupani mwao. Ezéchiel 22.27 Psaumes 53.4 Ezéchiel 34.3 Jean 15.18-15.19 Romains 12.9
3 Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama nyama sufuriani. Psaumes 14.4 Ezéchiel 11.6-11.7 Ezéchiel 11.3 Sophonie 3.3
4 Ndipo watakapomwomba Bwana, asiwaitikie; naam, atawaficha uso wake wakati huo, kwa kadiri walivyotenda mabaya kwa matendo yao. Esaïe 1.15 Proverbes 1.28 Psaumes 18.41 Matthieu 7.22 Ezéchiel 8.18
5 Bwana asema hivi katika habari za manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita. Jérémie 14.14-14.15 Esaïe 9.15-9.16 Jérémie 23.32 Matthieu 7.15 Jérémie 28.15-28.17
6 Kwa hiyo itakuwa usiku kwenu, msipate kuona maono; tena itakuwa giza kwenu, msiweze kubashiri; nalo jua litawachwea manabii, nao mchana utakuwa mweusi juu yao. Esaïe 8.20-8.22 Esaïe 29.10 Esaïe 59.10 Amos 8.9-8.10 Psaumes 74.9
7 Na hao waonaji watatahayarika, na wenye kubashiri watafadhaika; naam, hao wote watajifunika midomo yao; kwa maana; hapana jawabu la Mungu. Esaïe 44.25 Zacharie 13.4 Ezéchiel 24.17 1 Samuel 28.6 Esaïe 47.12-47.14
8 Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa roho ya Bwana; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubiri Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake. Esaïe 58.1 1 Corinthiens 2.12-2.13 1 Corinthiens 2.4 Jérémie 1.18 Jérémie 6.11
9 Sikieni haya, tafadhali, enyi vichwa vya nyumba ya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli, mnaochukia hukumu, na kuipotosha adili. Esaïe 1.23 Psaumes 58.1-58.2 Lévitique 26.15 Osée 5.1 Michée 3.1
10 Wanaijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. Ezéchiel 22.25-22.28 Jérémie 22.13-22.17 Habakuk 2.9-2.12 Matthieu 27.25 Sophonie 3.3
11 Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea Bwana, na kusema, Je! Hayupo Bwana katikati yetu? Hapana neno baya lo lote litakalotufikia. Esaïe 1.23 Jérémie 6.13 Jérémie 7.4 Michée 3.5 Esaïe 48.2
12 Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni. Jérémie 26.18 Psaumes 79.1 Michée 4.1-4.2 Psaumes 107.34 Michée 1.6

Cette Bible est dans le domaine public.