Partage du pays promis
Territoire encore à conquérir
1 Basi Yoshua alipokuwa mzee, na kwendelea sana miaka yake, Bwana akamwambia, Wewe umekuwa mzee na kwendelea sana miaka yako, kisha inasalia nchi nyingi sana bado kumilikiwa.
Josué 14.10 Deutéronome 31.3 1 Rois 1.1 Josué 24.29 Luc 1.7
2 Nchi iliyosalia ni hii; nchi zote za Wafilisti, na Wageshuri wote;
Josué 13.11 Juges 3.1 Joël 3.4 1 Samuel 27.8 Deutéronome 11.23-11.24
3 kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; mashehe matano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
Jérémie 2.18 Deutéronome 2.23 Juges 3.3 Sophonie 2.4-2.5 1 Samuel 6.4
4 upande wa kusini; nchi yote ya Wakanaani na Meara iliyo ya Wasidoni, mpaka Afeka, hata mpaka wa Waamori;
Josué 19.30 Juges 1.34-1.36 1 Samuel 4.1 Josué 12.7-12.8 Josué 10.40
5 na nchi ya Wagebali na Lebanoni yote, upande wa kuelekea maawio ya jua, kutoka Baal-gadi ulio chini ya mlima wa Hermoni mpaka kufikilia maingilio ya Hamathi;
1 Rois 5.18 Josué 12.7 Ezéchiel 27.9 Psaumes 83.7 Josué 11.17
6 na watu wote wenye kuikaa nchi ya vilima kutoka Lebanoni hata Misrefoth-maimu, maana, hao Wasidoni wote; hao wote nitawafukuza watoke mbele ya wana wa Israeli; lakini wewe uwape Israeli kuwa ni urithi wao, kama nilivyokuamuru.
Josué 11.8 Josué 23.13 Juges 2.21-2.23 Nombres 33.54 Genèse 15.18-15.21
7 Basi sasa gawanya nchi hii, iwe urithi wa hizi kabila kenda, na nusu ya kabila ya Manase.
Nombres 32.2-32.14 Ezéchiel 47.13-47.23 Nombres 33.54 Nombres 26.53-26.56 Ezéchiel 48.23-48.29
Partage du pays à l’est du Jourdain
8 Pamoja na yeye, Wareubeni na Wagadi walipata urithi wao, waliopewa na Musa, huko ng’ambo ya Yordani upande wa mashariki, vile vile kama huyo Musa mtumishi wa Bwana alivyowapa;
Josué 12.6 Josué 4.12 Nombres 32.33-32.42 Josué 22.4 Deutéronome 3.12-3.17
9 kutoka huko Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Amoni, na huo mji ulio pale katikati ya bonde, na nchi tambarare yote ya Medeba mpaka Diboni;
Nombres 21.30 Josué 13.16 Jérémie 48.18 Josué 12.2 Deutéronome 3.16
10 na miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala katika Heshboni, hata mpaka wa wana wa Amoni;
Nombres 21.24-21.26
11 na Gileadi na mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na mlima wa Hermoni wote, na Bashani yote mpaka Saleka;
1 Chroniques 2.23 Deutéronome 4.47-4.48 Josué 12.2-12.5
12 ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza.
Josué 12.4 Nombres 21.23-21.35 Josué 14.3-14.4 Deutéronome 3.10-3.11
13 Pamoja na hayo wana wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri, wala Wamaaka; lakini Wageshuri na Wamaaka wamekaa kati ya Israeli, hata siku hii ya leo.
Josué 13.11 Juges 2.1-2.3 Nombres 33.55 Josué 23.12-23.13 2 Samuel 13.37-13.38
14 Lakini hakuwapa watu wa kabila ya Lawi urithi uwao wote; maana sadaka za Bwana, Mungu wa Israeli, zisongezwazo kwa njia ya moto ndizo urithi wake huyo, kama alivyomwambia.
Josué 14.3-14.4 Nombres 18.20-18.24 Deutéronome 10.9 Deutéronome 12.19 Deutéronome 12.12
15 Musa akawapa kabila ya wana wa Reubeni kwa kadiri ya jamaa zao.
16 Mpaka wao ulikuwa kutoka hapo Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Arnoni, na huo mji ulio katikati ya bonde, na nchi tambarare yote iliyo karibu na Medeba;
Josué 13.9 Josué 12.2 Deutéronome 3.12 Nombres 21.28-21.30 Esaïe 15.1-15.2
17 na Heshboni na miji yake yote iliyoko katika bonde; na Diboni, na Bamoth-baali, na Beth-baal-meoni;
Nombres 21.19 Nombres 22.41 Nombres 32.38
18 na Yahasa, na Kedemothi, na Mefaathi;
Nombres 21.23 1 Chroniques 6.78-6.79 Josué 21.36-21.37
19 na Kiriathaimu, na Sibma, na Sereth-shahari katika kilima cha hilo bonde;Nombres 32.37-32.38
20 na Beth-peori, na nchi za matelemko ya Pisga, na Beth-yeshimothi;
Deutéronome 4.46 Josué 12.3 Deutéronome 3.17 Nombres 25.3 Ezéchiel 25.9
21 na miji yote ya nchi tambarare, na ufalme wote wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akitawala katika Heshboni, aliyepigwa na Musa pamoja na hao wakubwa wa Midiani, nao ni Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao mashehe wa Sihoni, waliokuwa katika nchi hiyo.
Nombres 31.8 Deutéronome 3.10 Nombres 21.24-21.35 Deutéronome 2.30-2.36
22 Balaamu naye, huyo mwana wa Beori, huyo mchawi, wana wa Israeli walimwua kwa upanga kati ya hao wengine waliowaua.
Nombres 31.8 Apocalypse 19.20 Jude 1.11 Nombres 22.5-22.7 Apocalypse 2.14
23 Na mpaka wa wana wa Reubeni ulikuwa ni mto wa Yordani, na mpaka wake. Huo ndio urithi wa wana wa Reubeni sawasawa na jamaa zao, miji yake na vijiji vyake.
24 Musa akawapa kabila ya Gadi, hao wana wa Gadi, kwa kadiri ya jamaa zao.
Nombres 32.34-32.36
25 Mpaka wao ulikuwa ni Yazeri, na miji hiyo ya Gileadi, na nusu ya nchi ya wana wa Amoni, mpaka Aroeri uliokabili Raba;
2 Samuel 11.1 Nombres 32.35 Deutéronome 3.11 2 Samuel 12.26 Nombres 21.26-21.30
26 tena kutoka Heshboni mpaka Ramath-Mizpe, na Betonimu; tena kutoka Mahanaimu hata mpaka wa Debiri;
2 Samuel 17.27 2 Samuel 2.8 Josué 20.8 Juges 10.17 Juges 11.29
27 tena katika bonde, Beth-haramu, na Bethnimira, na Sukothi, na Safoni, hiyo iliyosalia ya ufalme wa Sihoni mfalme wa Heshboni, yaani mto wa Yordani na mpaka wake, mpaka mwisho wa bahari ya Kinerethi ng’ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki.
Genèse 33.17 Nombres 34.11 Nombres 32.36 Deutéronome 3.17 Josué 11.2
28 Huo ndio urithi wa wana wa Gadi sawasawa na jamaa zao, miji yake na vijiji vyake.
29 Kisha Musa akawapa hao wa nusu ya kabila ya Manase urithi wao; ulikuwa ni wa hiyo nusu ya kabila ya wana wa Manase sawasawa na jamaa zao.
30 Na mpaka wao ulikuwa kutoka huko Mahanaimu, Bashani yote, na ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, na miji yote ya Yairi, iliyo katika Bashani, miji sitini;
Josué 13.26 1 Chroniques 2.21-2.23 Nombres 32.39-32.41 Deutéronome 3.13-3.15
31 na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase maana, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao.
Josué 12.4 Nombres 32.39-32.40
32 Hizi ndizo mirathi ambazo Musa alizigawanya katika nchi tambarare za Moabu, ng’ambo ya pili ya Yordani, kukabili Yeriko, upande wa mashariki.
33 Lakini Musa hakuwapa kabila ya Lawi urithi uwao wote; yeye Bwana, Mungu wa Israeli, ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.
Josué 18.7 Josué 13.14 Deutéronome 10.9 Deutéronome 18.1-18.2 Nombres 18.20