Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Juges 3.10
Bible en Swahili de l’est


1 Basi haya ndiyo mataifa ambao Bwana aliwaacha, ili awajaribu Israeli kwa hao, yaani, awajaribu hao wote ambao hawakuvijua vita vyote vya Kanaani;Juges 2.21-2.22 1 Pierre 4.12 Juges 2.10 Job 23.10 Deutéronome 7.22
2 ili kwamba vizazi vya wana wa Israeli wapate kujua ili kuwafundisha vita, hasa wao ambao hawakujua vita kabla ya wakati ule;Ephésiens 6.11-6.18 Matthieu 10.34-10.39 1 Timothée 6.12 Genèse 3.5 2 Timothée 2.3
3 aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi.Josué 13.3 Josué 13.5 Juges 18.7 Juges 10.7 1 Samuel 29.2
4 Naye aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao, apate kujua kwamba watasikiliza amri za Bwana, alizowaamuru baba zao, kwa mkono wa Musa.Juges 3.1 Juges 2.22 2 Thessaloniciens 2.9-2.12 Exode 15.25 1 Corinthiens 11.19
5 Basi wana wa Israeli wakaketi kati ya Wakanaani; hao Wahiti, na hao Waamori, na hao Waperizi, na hao Wahivi na hao Wayebusi;Psaumes 106.34-106.38 Exode 3.8 Genèse 10.15-10.18 Genèse 15.19-15.21 Deutéronome 7.1
6 wakawaoa binti zao, na binti zao wenyewe wakawaoza wana wao waume, na kuitumikia miungu yao.Exode 34.16 Deutéronome 7.3-7.4 Néhémie 13.23-13.27 Esdras 9.11-9.12 Ezéchiel 16.3
7 Wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakamsahau Bwana, Mungu wao, nao wakawatumikia Mabaali na Maashtorethi.Exode 34.13 Juges 2.11-2.13 Juges 6.25 Juges 3.12 2 Chroniques 34.3
8 Kwa hiyo hasira za Bwana ziliwaka juu ya Israeli, naye akawauza na kuwatia mikononi mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia; na wana wa Israeli wakamtumikia huyo Kushan-rishathaimu muda wa miaka minane.Juges 2.14 Habakuk 3.7 Juges 2.20 Psaumes 6.1 Exode 22.24
9 Kisha wana wa Israeli walipomlingana Bwana, Bwana akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.Juges 1.13 Juges 3.15 Juges 10.10 Juges 6.7 Néhémie 9.27
10 Roho ya Bwana ikamjilia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka kwenenda vitani, naye Bwana akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu.Juges 13.25 Juges 11.29 Juges 14.19 Juges 6.34 Juges 14.6
11 Nayo nchi ikawa na amani muda wa miaka arobaini. Kisha Othnieli, mwana wa Kenazi, akafa.Josué 11.23 Juges 8.28 Juges 5.31 Juges 3.30 Esther 9.22
12 Basi wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu tena mbele za Bwana; naye Bwana akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu juu ya Israeli, kwa sababu walikuwa wameyafanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana.1 Samuel 12.9 Juges 2.19 Daniel 5.18 Esaïe 45.1-45.4 Ezéchiel 38.16
13 Huyo Egloni akakutanisha kwake wana wa Amoni na Amaleki; akaenda na kuwapiga Israeli, nao wakauchukua huo mji wa mitende.Juges 1.16 Deutéronome 34.3 Psaumes 83.6-83.7 Juges 5.14
14 Wana wa Israeli walimtumikia Egloni mfalme wa Moabu muda wa miaka kumi na minane.Deutéronome 28.47-28.48 Deutéronome 28.40 Lévitique 26.23-26.25
15 Lakini wana wa Israeli walipomlilia Bwana, Bwana akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi.Psaumes 78.34 Juges 3.9 Juges 20.16 1 Chroniques 12.2 Esaïe 36.16
16 Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kuume.Psaumes 45.3 Psaumes 149.6 Apocalypse 1.16 Apocalypse 2.12 Cantique 3.8
17 Kisha akamsongezea Egloni, mfalme wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu aliyewanda sana.Jérémie 5.28 Ezéchiel 34.20 Psaumes 73.7 Job 15.27 Juges 3.29
18 Naye hapo alipokuwa amekwisha kuisongeza hiyo tunu, akawapa ruhusa watu hao walioichukua tunu, wakaenda zao. 19 Lakini yeye mwenyewe akageuka kutoka huko kwenye sanamu zilizokuwa karibu na Gilgali, akasema, Mimi nina ujumbe wa siri kwako wewe, Ee mfalme. Naye akasema, Nyamazeni kimya. Watu wote waliokuwa wanasimama karibu naye wakatoka na kumwacha.Josué 4.20 2 Rois 9.5-9.6 Juges 3.20 Actes 23.18-23.19 Genèse 45.1
20 Basi Ehudi akamwendea; naye alikuwa anaketi peke yake katika chumba chake cha baridi. Ehudi akasema, Mimi nina ujumbe utokao kwa Mungu kwako wewe. Basi akainuka katika kiti chake.Amos 3.15 Psaumes 29.1 Juges 3.19 Jérémie 10.7 Michée 6.9
21 Ehudi akaunyosha mkono wake wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kuume, akamtia tumboni mwake;1 Samuel 15.33 Job 20.25 2 Corinthiens 5.16 Nombres 25.7-25.8 Zacharie 13.3
22 hicho kipini nacho kikaingia ndani pamoja na huo upanga wenyewe; nayo mafuta yakashikamana tena juu ya upanga, kwani hakuutoa tena upanga tumboni; nao ukatokea kwa nyuma. 23 Ndipo Ehudi akatoka nje barazani, akamfungia milango ya hicho chumba na kuifunga kwa ufunguo. 24 Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi amejifunika miguu yake ndani ya chumba cha baridi.1 Samuel 24.3
25 Wakangoja hata wakatahayari; na tazama, hakuifungua milango ya chumba; basi wakatwaa ufunguo, na kuifungua; na tazama, bwana wao alikuwa ameanguka nchi, naye amekufa. 26 Naye Ehudi alikimbia hapo walipokuwa wakingoja, akapita huko kwenye sanamu, na kukimbilia Seira. 27 Ikawa, hapo alipofika akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, ndipo wana wa Israeli wakatelemka pamoja naye kutoka huko milimani, naye akawatangulia.Juges 6.34 1 Samuel 13.3 Juges 17.1 Juges 5.14 2 Rois 9.13
28 Akawaambia, Niandameni mimi; kwa kuwa Bwana amewatia adui zenu, Wamoabi, mikononi mwenu. Basi wakatelemka na kumfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha Wamoabi, wala hawakumwacha mtu kuvuka.Juges 12.5 Juges 7.9 Josué 2.7 Juges 7.15 Juges 7.24
29 Wakati huo wakapiga katika Wamoabi watu waume wapata kama elfu kumi, ambao wote walikuwa wanene, na wote mashujaa; hakupona hata mtu mmoja.Job 15.27 Juges 3.17 Psaumes 17.10 Deutéronome 32.15
30 Basi Moabu alishindwa siku hiyo chini ya mikono ya Israeli. Nayo nchi ikawa na amani muda wa miaka themaniniJuges 3.11 Juges 5.31
31 Tena baada yake huyo alikuwapo Shamgari mwana wa Anathi, aliyepiga katika Wafilisti watu mia sita kwa konzo la ng’ombe; yeye naye aliwaokoa Israeli.Juges 5.6 1 Samuel 17.47 Juges 2.16 1 Corinthiens 1.17 Juges 5.8

Cette Bible est dans le domaine public.