Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 30.3
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, nitakutukuza kwa maana umeniinua, Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu. 2 Ee Bwana, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya. 3 Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni. 4 Mwimbieni Bwana zaburi, Enyi watauwa wake. Na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake. 5 Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha. 6 Nami nilipofanikiwa nalisema, Sitaondoshwa milele. 7 Bwana, kwa radhi yako Wewe uliuimarisha mlima wangu. Uliuficha uso wako, Nami nikafadhaika. 8 Ee Bwana, nalikulilia Wewe, Naam, kwa Bwana naliomba dua. 9 Mna faida gani katika damu yangu Nishukapo shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yataitangaza kweli yako? 10 Ee Bwana, usikie, unirehemu, Bwana, uwe msaidizi wangu. 11 Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha. 12 Ili utukufu wangu ukusifu, Wala usinyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, Nitakushukuru milele.

Cette Bible est dans le domaine public.