Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 132
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana, umkumbukie Daudi Taabu zake zote alizotaabika. Psaumes 121.1 Psaumes 120.1 Exode 2.24 Psaumes 129.1 1 Samuel 18.1-18.30
2 Ndiye aliyemwapia Bwana, Akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo. Genèse 49.24 Psaumes 50.1 Esaïe 49.26 Psaumes 146.5-146.6 Psaumes 56.12
3 Sitaingia hemani mwa nyumba yangu, Wala sitapanda matandiko ya kitanda changu; Ecclésiaste 9.10 Matthieu 6.33 Aggée 1.4
4 Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi, Wala kope zangu kusinzia; Proverbes 6.4 Ruth 3.18 Genèse 24.33
5 Hata nitakapompatia Bwana mahali, Na Shujaa wa Yakobo maskani. 1 Chroniques 22.7 Ephésiens 2.22 1 Rois 8.27 Actes 7.46-7.49 2 Chroniques 2.6
6 Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata, Katika konde la Yearimu tuliiona. 1 Samuel 17.12 1 Samuel 7.1 Michée 5.2 Ruth 1.2 Genèse 35.19
7 Na tuingie katika maskani yake, Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake. Psaumes 99.5 Psaumes 5.7 Esaïe 2.3 Psaumes 122.1 Psaumes 95.6
8 Ee Bwana, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako. 2 Chroniques 6.41-6.42 Psaumes 68.1 Nombres 10.35-10.36 Psaumes 78.61
9 Makuhani wako na wavikwe haki, Watauwa wako na washangilie. Job 29.14 Esaïe 61.10 Psaumes 132.16 Esdras 3.11-3.12 1 Pierre 5.5
10 Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako, Usiurudishe nyuma uso wa masihi 2 Rois 19.34 1 Rois 11.34 Psaumes 89.38-89.39 Psaumes 84.9 1 Rois 15.4-15.5
11 Bwana amemwapia Daudi neno la kweli, Hatarudi nyuma akalihalifu, Baadhi ya wazao wa mwili wako Nitawaweka katika kiti chako cha enzi. 2 Samuel 7.12 2 Chroniques 6.16 Actes 2.30 Psaumes 110.4 Psaumes 89.3-89.4
12 Wanao wakiyashika maagano yangu, Na shuhuda nitakazowafundisha; Watoto wao nao wataketi Katika kiti chako cha enzi milele. Psaumes 89.30-89.35 Esaïe 59.21 Actes 2.30 Psaumes 115.14 Psaumes 102.28
13 Kwa kuwa Bwana ameichagua Sayuni, Ameitamani akae ndani yake. Psaumes 68.16 Psaumes 76.1-76.2 Psaumes 78.68-78.69 Hébreux 12.22 Psaumes 48.1-48.3
14 Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele, Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani. Esaïe 66.1 Psaumes 132.8 Psaumes 68.18 1 Rois 8.13 Psaumes 87.2
15 Hakika nitavibariki vyakula vyake Wahitaji wake nitawashibisha chakula. Psaumes 147.14 Matthieu 14.19-14.21 Psaumes 22.26 Proverbes 3.9-3.10 Exode 23.25
16 Na makuhani wake nitawavika wokovu, Na watauwa wake watashangilia. 2 Chroniques 6.41 Psaumes 132.9 Zacharie 9.9 Esaïe 61.10 Osée 11.12
17 Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi wangu. Ezéchiel 29.21 Luc 1.69 2 Chroniques 21.7 1 Rois 11.36 1 Rois 15.4
18 Adui zake nitawavika aibu, Bali juu yake taji yake itasitawi. Job 8.22 Psaumes 109.29 Psaumes 35.26 Psaumes 21.8-21.9 Esaïe 9.6-9.7

Cette Bible est dans le domaine public.