Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 30
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, nitakutukuza kwa maana umeniinua, Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu. Psaumes 25.2 Psaumes 35.19 2 Samuel 6.20 Psaumes 28.9 Psaumes 13.4
2 Ee Bwana, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya. Psaumes 6.2 Psaumes 103.3-103.4 Psaumes 88.13 Exode 15.26 Genèse 20.17
3 Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni. Psaumes 28.1 Psaumes 16.10 Psaumes 86.13 Job 33.19-33.22 Jonas 2.4-2.6
4 Mwimbieni Bwana zaburi, Enyi watauwa wake. Na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake. Psaumes 97.12 1 Chroniques 16.4 Psaumes 135.19-135.21 Apocalypse 4.8 Exode 15.11
5 Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha. Esaïe 54.7-54.8 2 Corinthiens 4.17 Psaumes 103.9 Esaïe 26.20 Psaumes 6.6-6.9
6 Nami nilipofanikiwa nalisema, Sitaondoshwa milele. Daniel 4.30 Psaumes 10.6 Psaumes 16.8 Esaïe 56.12 Luc 12.19
7 Bwana, kwa radhi yako Wewe uliuimarisha mlima wangu. Uliuficha uso wako, Nami nikafadhaika. Psaumes 104.29 Psaumes 143.7 Deutéronome 31.17 Job 30.26-30.31 Psaumes 10.1
8 Ee Bwana, nalikulilia Wewe, Naam, kwa Bwana naliomba dua. Philippiens 4.6-4.7 1 Corinthiens 12.8-12.9 Psaumes 77.1-77.2 Psaumes 34.6 Psaumes 130.1-130.2
9 Mna faida gani katika damu yangu Nishukapo shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yataitangaza kweli yako? Psaumes 6.5 Psaumes 88.10-88.12 Psaumes 115.17-115.18 Psaumes 118.17 Esaïe 38.18
10 Ee Bwana, usikie, unirehemu, Bwana, uwe msaidizi wangu. Psaumes 54.4 Psaumes 51.1-51.2 Psaumes 28.7 Psaumes 143.1 Psaumes 27.7
11 Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha. Jérémie 31.4 Psaumes 150.4 Apocalypse 21.4 Psaumes 149.3 Ecclésiaste 3.4
12 Ili utukufu wangu ukusifu, Wala usinyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, Nitakushukuru milele. Psaumes 16.9 Psaumes 57.8 Psaumes 71.14 Genèse 49.6 Psaumes 146.1-146.2

Cette Bible est dans le domaine public.