Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 122.7 Bible en Swahili de l’est
Vœux pour la paix de Jérusalem
1 Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana. 2 Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu. 3 Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana, 4 Huko ndiko walikopanda kabila, Kabila za Bwana; Ushuhuda kwa Israeli, Walishukuru jina la Bwana. 5 Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya mbari ya Daudi. 6 Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao; 7 Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako. 8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe. 9 Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu, Nikutafutie mema.