Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 64.1 Bible en Swahili de l’est
Punition des méchants
1 Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu; Unilinde uhai wangu na hofu ya adui. 2 Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya, Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu; 3 Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu, 4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi. 5 Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Husema, Ni nani atakayeiona? 6 Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili; Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao, Na moyo wake, huwa siri kabisa. 7 Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha, Kwa mshale mara watapigwa. 8 Ndivyo watakavyokwazwa, Ulimi wao wenyewe ukishindana nao. Wote wawaonao watatikisa kichwa. 9 Na watu wote wataogopa, Wataitangaza kazi ya Mungu, Na kuyafahamu matendo yake. 10 Mwenye haki atamfurahia Bwana na kumkimbilia, Na wote wenye moyo wa adili watajisifu.