Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 53.2 Bible en Swahili de l’est
1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.2 Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.3 Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja. 4 Je! Wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawakumwita MUNGU. 5 Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu, Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru. Umewatia aibu, Kwa sababu MUNGU amewadharau. 6 Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! MUNGU awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.