1 Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu; Unilinde uhai wangu na hofu ya adui.
Psaumes 56.2-56.4 Psaumes 55.1-55.2 Psaumes 130.1-130.2 Actes 18.9-18.10 Psaumes 27.7
2 Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya, Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;Jérémie 11.19 Psaumes 56.6 Psaumes 27.5 Matthieu 26.3-26.4 Psaumes 109.2-109.3
3 Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,
Psaumes 58.7 Psaumes 11.2 Psaumes 57.4 Esaïe 54.17 Proverbes 30.14
4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.
Psaumes 55.19 Psaumes 10.8-10.9 Habakuk 3.14 1 Pierre 2.22-2.23 Jean 19.6
5 Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Husema, Ni nani atakayeiona?
Psaumes 10.11 Psaumes 140.5 Exode 15.9 Proverbes 1.11-1.14 Ezéchiel 8.12
6 Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili; Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao, Na moyo wake, huwa siri kabisa.
Proverbes 20.5 1 Samuel 25.10 1 Corinthiens 4.5 Psaumes 35.11 Psaumes 49.11
7 Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha, Kwa mshale mara watapigwa.
Psaumes 7.12-7.13 Matthieu 24.50-24.51 Proverbes 6.15 Deutéronome 32.23 Esaïe 30.13
8 Ndivyo watakavyokwazwa, Ulimi wao wenyewe ukishindana nao. Wote wawaonao watatikisa kichwa.
Proverbes 18.7 Proverbes 12.13 Nahum 3.7 Luc 19.22 Jérémie 18.16
9 Na watu wote wataogopa, Wataitangaza kazi ya Mungu, Na kuyafahamu matendo yake.
Jérémie 51.10 Jérémie 50.28 Psaumes 40.3 Psaumes 58.11 Apocalypse 11.13
10 Mwenye haki atamfurahia Bwana na kumkimbilia, Na wote wenye moyo wa adili watajisifu.
Psaumes 32.11-33.1 Psaumes 68.2-68.3 Psaumes 40.3 Psaumes 58.10 Job 22.19