Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 64
Bible en Swahili de l’est


1 Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu; Unilinde uhai wangu na hofu ya adui. Psaumes 143.1-143.3 Actes 27.24 Psaumes 31.13-31.15 Psaumes 56.2-56.4 Psaumes 55.1-55.2
2 Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya, Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu; Jérémie 11.19 Psaumes 56.6 Jérémie 18.23 Psaumes 27.5 Matthieu 26.3-26.4
3 Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu, Psaumes 58.7 Psaumes 11.2 Psaumes 57.4 Jacques 3.6-3.8 Jérémie 9.3
4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi. Psaumes 55.19 1 Samuel 19.10 Néhémie 4.11 2 Samuel 15.14 Psaumes 10.8-10.9
5 Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Husema, Ni nani atakayeiona? Psaumes 10.11 Psaumes 140.5 Nombres 22.6 Apocalypse 11.10 Matthieu 26.3-26.4
6 Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili; Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao, Na moyo wake, huwa siri kabisa. Jean 18.29-18.30 1 Samuel 22.9 Psaumes 5.9 Proverbes 20.5 1 Samuel 25.10
7 Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha, Kwa mshale mara watapigwa. Psaumes 7.12-7.13 1 Thessaloniciens 5.2-5.3 Psaumes 73.19 1 Rois 22.34 Matthieu 24.50-24.51
8 Ndivyo watakavyokwazwa, Ulimi wao wenyewe ukishindana nao. Wote wawaonao watatikisa kichwa. Proverbes 18.7 Proverbes 12.13 Jérémie 48.27 Psaumes 140.9 Nahum 3.7
9 Na watu wote wataogopa, Wataitangaza kazi ya Mungu, Na kuyafahamu matendo yake. Jérémie 51.10 Jérémie 50.28 Psaumes 40.3 Psaumes 107.42-107.43 Ezéchiel 14.23
10 Mwenye haki atamfurahia Bwana na kumkimbilia, Na wote wenye moyo wa adili watajisifu. Psaumes 97.11 Psaumes 11.1 Psaumes 32.11-33.1 Psaumes 68.2-68.3 Psaumes 40.3

Cette Bible est dans le domaine public.