Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jérémie 47
Bible en Swahili de l’est


1 Neno la Bwana lililomjia Yeremia, nabii, katika habari za Wafilisti, kabla Farao hajapiga Gaza. Jérémie 25.20 Genèse 10.19 Zacharie 9.5-9.7 1 Rois 4.24 Amos 1.6-1.8
2 Bwana asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi watapiga yowe. Jérémie 46.20 Esaïe 15.2-15.5 Jérémie 8.16 Jérémie 1.14 Esaïe 8.7-8.8
3 Kwa sababu ya mshindo wa kukanyaga kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbiombio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya ngurumo ya magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu; Juges 5.22 Jérémie 8.16 Deutéronome 28.54-28.55 Lamentations 4.3-4.4 Ezéchiel 26.10-26.11
4 kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana Bwana atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori. Amos 9.7 Deutéronome 2.23 Esaïe 20.6 Amos 1.8-1.10 Ezéchiel 21.25
5 Upaa umeupata Gaza; Ashkeloni umenyamazishwa Mabaki ya bonde lao; Hata lini utajikata-kata? Jérémie 48.37 Jérémie 25.20 Jérémie 41.5 Michée 1.16 Jérémie 16.1
6 Ee upanga wa Bwana, Siku ngapi zitapita kabla hujatulia? Ujitie katika ala yako; Pumzika, utulie. Jérémie 12.12 Ezéchiel 21.3-21.5 Jérémie 25.27 Ezéchiel 14.17 Jérémie 4.21
7 Utawezaje kutulia, Ikiwa Bwana amekupa agizo? Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani, Ndipo alipoyaamuru hayo. Ezéchiel 14.17 Michée 6.9 Esaïe 10.6 1 Samuel 15.3 Esaïe 13.3

Cette Bible est dans le domaine public.