Prophétie sur les Philistins
1 Neno la Bwana lililomjia Yeremia, nabii, katika habari za Wafilisti, kabla Farao hajapiga Gaza.
Jérémie 25.20 Genèse 10.19 Zacharie 9.5-9.7 1 Rois 4.24 Sophonie 2.4-2.7
2 Bwana asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi watapiga yowe.
Jérémie 8.16 Jérémie 1.14 Esaïe 8.7-8.8 Jérémie 46.20 Esaïe 15.2-15.5
3 Kwa sababu ya mshindo wa kukanyaga kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbiombio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya ngurumo ya magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;
Jérémie 8.16 Juges 5.22 Jérémie 46.9 Nahum 3.2-3.3 Deutéronome 28.54-28.55
4 kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana Bwana atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.
Amos 9.7 Esaïe 20.6 Deutéronome 2.23 Amos 1.8-1.10 Ezéchiel 21.29
5 Upaa umeupata Gaza; Ashkeloni umenyamazishwa Mabaki ya bonde lao; Hata lini utajikata-kata?Jérémie 48.37 Jérémie 25.20 Jérémie 41.5 Michée 1.16 Deutéronome 14.1
6 Ee upanga wa Bwana, Siku ngapi zitapita kabla hujatulia? Ujitie katika ala yako; Pumzika, utulie.
Ezéchiel 21.3-21.5 Jérémie 12.12 Ezéchiel 21.30 Jérémie 15.3 Deutéronome 32.41-32.42
7 Utawezaje kutulia, Ikiwa Bwana amekupa agizo? Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani, Ndipo alipoyaamuru hayo.
Michée 6.9 Ezéchiel 14.17 Esaïe 10.6 Sophonie 2.6-2.7 Amos 3.6