Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Samuel 5.8
Bible en Swahili de l’est


1 Basi Wafilisti walikuwa wamelichukua sanduku la Mungu, wakaenda nalo kutoka Eben-ezeri hata Ashdodi.1 Samuel 7.12 1 Samuel 4.1 Josué 13.3 1 Samuel 4.11 Psaumes 78.61
2 Wafilisti wakalichukua sanduku la Mungu, wakalitia katika nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na Dagoni.Juges 16.23 1 Chroniques 10.10 Habakuk 1.16 Daniel 5.2 Daniel 5.23
3 Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la Bwana. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena.Esaïe 46.1-46.2 Esaïe 19.1 Esaïe 46.7 Esaïe 41.7 Sophonie 2.11
4 Hata walipoamka kesho yake asubuhi, kumbe! Dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la Bwana; na kichwa chake Dagoni na vitanga vya mikono yake vyote viwili vimekatika, vipo vimelala kizingitini; Dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu.Michée 1.7 Jérémie 50.2 Jérémie 10.11 Esaïe 27.9 Daniel 11.8
5 Kwa hiyo makuhani wa Dagoni, na mtu awaye yote aingiaye nyumbani mwa Dagoni, hawakanyagi kizingiti cha nyumba ya Dagoni huko Ashdodi, hata leo.Sophonie 1.9 Josué 5.15 Psaumes 115.4-115.7 Psaumes 135.15-135.18
6 Lakini mkono wa Bwana ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi, akawaharibu, akawapiga kwa majipu, huko Ashdodi na mipakani mwake.1 Samuel 5.11 Exode 9.3 Psaumes 32.4 Actes 13.11 Psaumes 78.66
7 Kisha hao watu wa Ashdodi, walipoona ilivyokuwa, walisema, Hilo sanduku la Mungu wa Israeli halitakaa kwetu; kwa maana mkono wake ni mzito juu yetu, na juu ya Dagoni, mungu wetu.Exode 9.28 1 Samuel 4.8 1 Chroniques 15.13 Jérémie 48.7 Exode 10.7
8 Basi wakatuma watu waende kuwakusanya kwao mashehe wote wa Wafilisti, wakasema, Tulifanyieje sanduku la Mungu wa Israeli? Nao wakajibu, Sanduku la Mungu wa Israeli na lihamishwe liende Gathi. Wakalihamisha sanduku la Mungu wa Israeli.Amos 6.2 1 Samuel 17.4 Zacharie 12.3 1 Samuel 5.11
9 Ikawa, walipokwisha lihamisha, mkono wa Bwana ulikuwa juu ya mji huo, kwa kuwafadhaisha sana; akawapiga watu wa mjini, wadogo kwa wakubwa, wakapatwa na majipu.1 Samuel 5.6 Deutéronome 2.15 1 Samuel 7.13 1 Samuel 12.15 Psaumes 78.66
10 Basi, wakalipeleka sanduku la Mungu mpaka Ekroni. Ikawa, sanduku la Mungu lilipofika Ekroni, watu wa Ekroni walifanya kelele, wakasema, Wamelileta hilo sanduku la Mungu wa Israeli kwetu, hata kutuua sisi na watu wetu.Juges 1.18 Josué 15.45 Amos 1.8 2 Rois 1.2
11 Kwa hiyo wakatuma watu waende kuwakusanya mashehe wote wa Wafilisti, wakasema, Liondoeni hilo sanduku la Mungu wa Israeli, liende tena mahali pake, ili lisituue sisi, wala watu wetu; kwa sababu kulikuwa na fadhaa kubwa sana mjini mwote; mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko.1 Samuel 5.6 1 Samuel 5.8-5.9 Jérémie 48.42-48.44 Esaïe 13.7-13.9
12 Na wale wasiokufa walipigwa kwa yale majipu; na kilio cha mji kikafika mbinguni.Exode 12.30 Jérémie 25.34 1 Samuel 9.16 Amos 5.19 Jérémie 48.3

Cette Bible est dans le domaine public.