Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 125 Bible en Swahili de l’est
Dieu, un rempart pour son peuple
1 Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. 2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. 3 Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu. 4 Ee Bwana, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo. 5 Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, Bwana atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.