Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Chroniques 10
Bible en Swahili de l’est


1 Basi Wafilisti wakapigana juu ya Israeli; nao watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, wakaanguka wameuawa katika mlima Gilboa. 1 Samuel 31.1-31.13 1 Chroniques 10.8 2 Samuel 1.6 1 Samuel 28.1 1 Samuel 29.1-29.2
2 Nao Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe; Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli. Esaïe 57.1-57.2 1 Chroniques 9.39 2 Rois 25.7 1 Samuel 14.49 Exode 20.5
3 Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde. Genèse 49.23-49.24 1 Samuel 31.3-31.6 2 Samuel 1.4-1.10 Amos 2.14
4 Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao, wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia. 1 Samuel 31.4 1 Samuel 17.26 Matthieu 27.4-27.5 2 Samuel 1.14-1.16 1 Rois 16.18
5 Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa. 6 Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu; na nyumba yake yote wakafa pamoja. 1 Samuel 4.10-4.11 Ecclésiaste 9.1-9.2 Osée 13.10-13.11 1 Samuel 12.25 1 Samuel 4.18
7 Kisha watu wote wa Israeli, waliokuwa huko bondeni, walipoona ya kuwa wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo. Juges 6.2 Deutéronome 28.43 1 Samuel 13.6 Lévitique 26.31 1 Samuel 31.7
8 Hata ikawa siku ya pili yake Wafilisti walipokwenda kuwateka nyara hao waliouawa, walimwona Sauli na wanawe wameanguka juu ya mlima Gilboa. 2 Chroniques 20.25 2 Rois 3.23 1 Samuel 31.8
9 Wakamvua mavazi, wakamtwalia kichwa, na silaha zake, kisha wakapeleka wajumbe kwenda nchi ya Wafilisti pande zote, ili kutangaza habari kwa sanamu zao, na kwa watu. 1 Samuel 31.9-31.10 Daniel 5.2-5.4 2 Samuel 1.20 Juges 16.23-16.24 Matthieu 14.11
10 Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa miungu yao, wakakikaza kichwa chake nyumbani mwa Dagoni. 1 Samuel 31.10 1 Samuel 5.2-5.7
11 Na watu wote wa Yabesh-gileadi waliposikia hayo yote Wafilisti waliyomtenda Sauli, 1 Samuel 31.11-31.13 1 Samuel 11.1-11.11 2 Samuel 2.4-2.7
12 wakainuka mashujaa wote, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi, wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni huko Yabeshi, nao wakafunga muda wa siku saba. 2 Samuel 3.35 Genèse 35.8 2 Samuel 21.12-21.14 Genèse 50.10
13 Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, Lévitique 20.6 1 Samuel 15.23 Lévitique 19.31 Esaïe 8.19 Deutéronome 18.10-18.14
14 asiulize kwa Bwana; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese. 1 Samuel 15.28 1 Samuel 13.14 2 Samuel 3.9-3.10 1 Chroniques 12.23 1 Samuel 28.17

Cette Bible est dans le domaine public.