Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
2 Chroniques 3.3 Bible en Swahili de l’est
1 Ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, juu ya mlima Moria, pale Bwana alipomtokea Daudi babaye alipotengeza mahali pale alipoagiza Daudi, katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.1 Chroniques 21.18 Genèse 22.14 Genèse 22.2 1 Rois 6.1-6.14 1 Chroniques 22.1 2 Akaanza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa kutawala kwake.1 Rois 6.1 3 Basi hii ndiyo misingi ya majengo ya nyumba ya Mungu aliyoiweka Sulemani. Urefu wake kwa mikono ya cheo cha kwanza ulikuwa mikono sitini, na upana wake mikono ishirini.1 Rois 6.2-6.3 1 Chroniques 28.11-28.19 4 Na ukumbi uliokuwa mbele yake, urefu wake kadiri ya upana wa nyumba ulikuwa mikono ishirini, na kwenda juu kwake mia na ishirini; akaufunikiza ndani kwa dhahabu safi.Jean 10.23 Actes 5.12 Actes 3.11 5 Nayo nyumba kubwa akaifunika miti ya miberoshi, aliyoifunikiza kwa dhahabu safi, akaifanyizia mitende na minyororo.1 Rois 6.15-6.17 1 Rois 6.21-6.22 6 Akaipamba nyumba kwa vito iwe na uzuri; nayo dhahabu ilikuwa dhahabu ya Parvaimu.1 Chroniques 29.8 Apocalypse 21.18-21.21 Esaïe 54.11-54.12 1 Chroniques 29.2 7 Tena, akaifunikiza kwa dhahabu nyumba, na boriti, na vizingiti, na kuta zake, na milango yake; akachora makerubi kutani.1 Rois 6.20-6.22 1 Rois 6.29-6.35 Exode 26.29 Ezéchiel 7.20 Exode 26.1 8 Akaifanya nyumba ya patakatifu pa patakatifu; urefu wake kadiri ya upana wa nyumba, ulikuwa mikono ishirini, na upana wake mikono ishirini; akaifunikiza kwa dhahabu safi, ya talanta mia sita.Exode 26.33 Hébreux 9.3 Hébreux 10.19 1 Rois 6.16 1 Rois 6.19-6.20 9 Na uzani wa misumari ulikuwa shekeli hamsini za dhahabu. Akazifunikiza orofa zake za juu kwa dhahabu.1 Chroniques 28.11 10 Na ndani ya nyumba ya patakatifu pa patakatifu akafanyiza makerubi mawili ya kuchonga; wakayafunikiza kwa dhahabu.1 Rois 6.23-6.28 Exode 25.18 11 Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili. 12 Na bawa la kerubi la pili lilikuwa mikono mitano, likiufikilia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la kwanza. 13 Yakaenea mabawa ya makerubi hayo mikono ishirini; yakasimama juu ya miguu yao, na nyuso zao ziliielekea nyumba.Exode 25.20 14 Akalifanya pazia la samawi na urujuani na nyekundu, na kitani safi, akaifanyizia makerubi.Hébreux 9.3 Matthieu 27.51 Exode 26.31-26.35 Hébreux 10.20 15 Tena akafanya mbele ya nyumba nguzo mbili za mikono thelathini na tano kwenda juu kwake, na taji iliyokuwa juu yake moja moja ilikuwa mikono mitano.1 Rois 7.15-7.24 Jérémie 52.20-52.23 16 Akafanya minyororo ndani ya chumba cha ndani, akaiweka juu ya vichwa vya nguzo; akafanya makomamanga mia, akayaweka juu ya hiyo minyororo.1 Rois 7.20 1 Rois 6.21 17 Akazisimamisha nguzo hizo mbele ya hekalu, moja upande wa kuume, na ya pili upande wa kushoto; akaliita jina la ile ya kuume Yakini, na jina la ile ya kushoto Boazi.1 Rois 7.21