Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 120.1 Bible en Swahili de l’est
La souffrance de l’exilé
1 Katika shida yangu nalimlilia Bwana Naye akaniitikia. 2 Ee Bwana, uiponye nafsi yangu Na midomo ya uongo na ulimi wa hila. 3 Akupe nini, akuzidishie nini, Ewe ulimi wenye hila? 4 Mishale ya mtu hodari iliyochongoka, Pamoja na makaa ya mretemu. 5 Ole wangu mimi! Kwa kuwa nimekaa katika Mesheki; Na kufanya maskani yangu Katikati ya hema za Kedari. 6 Nafsi yangu imekaa siku nyingi, Pamoja naye aichukiaye amani. 7 Mimi ni wa amani; Bali ninenapo, wao huelekea vita.