Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 13
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, hata lini utanisahau, hata milele? Hata lini utanificha uso wako? 2 Hata lini nifanye mashauri nafsini mwangu, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Hata lini adui yangu atukuke juu yangu? 3 Ee Bwana, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti. 4 Adui yangu asije akasema, Nimemshinda; Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa. 5 Nami nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako. 6 Naam, nimwimbie Bwana, Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.

Cette Bible est dans le domaine public.