Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 142 Bible en Swahili de l’est
Prière dans la détresse
1 Kwa sauti yangu nitamlilia Bwana, Kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua. 2 Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake. 3 Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. 4 Utazame mkono wa kuume ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho. 5 Bwana, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai. 6 Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye nao wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi. 7 Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu.