Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 26
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini Bwana bila wasiwasi. Psaumes 7.8 Psaumes 28.7 Proverbes 20.7 2 Rois 20.3 Psaumes 94.18
2 Ee Bwana, unijaribu na kunipima; Unisafishe mtima wangu na moyo wangu. Psaumes 7.9 Psaumes 17.3 Psaumes 66.10 Zacharie 13.9 Job 31.4-31.6
3 Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako. 2 Rois 20.3 Ephésiens 4.20-4.25 Psaumes 86.11 Esaïe 8.20 3 Jean 1.11
4 Sikuketi pamoja na watu wa ubatili, Wala sitaingia mnamo wanafiki. Psaumes 1.1 Jérémie 15.17 Psaumes 119.115 Psaumes 119.63 Proverbes 13.20
5 Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu. Psaumes 31.6 Psaumes 139.21-139.22 Psaumes 1.1 Psaumes 101.3-101.8 1 Corinthiens 5.9-5.11
6 Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia, Na kuizunguka madhabahu yako, Ee Bwana Psaumes 73.13 Psaumes 43.4 Exode 30.19-30.20 1 Timothée 2.8 1 Corinthiens 11.28-11.29
7 Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu. Psaumes 9.1 Luc 19.37-19.40 1 Samuel 1.24 2 Chroniques 20.26-20.29 Psaumes 100.4-100.5
8 Bwana, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako. Luc 2.49 Jean 2.14-2.17 Psaumes 63.2-63.3 2 Samuel 15.25 Esaïe 38.22
9 Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu. Psaumes 139.19 Matthieu 25.46 Psaumes 51.14 Psaumes 55.23 2 Samuel 21.1
10 Mikononi mwao mna madhara, Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa. Deutéronome 16.19 1 Samuel 8.3 Exode 23.8 Michée 2.1-2.3 Amos 5.12
11 Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; Unikomboe, unifanyie fadhili. Psaumes 69.18 Psaumes 26.1 Néhémie 5.15 Esaïe 38.3 Psaumes 49.7
12 Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika makusanyiko nitamhimidi Bwana. Psaumes 27.11 Psaumes 40.2 Psaumes 111.1 Proverbes 10.9 Psaumes 26.7

Cette Bible est dans le domaine public.