Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 4.2 Bible en Swahili de l’est
La sécurité qu’accorde l’Éternel
1 Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Umenifanyizia nafasi wakati wa shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu. 2 Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo? 3 Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa; Bwana atasikia nimwitapo. 4 Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia. 5 Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana. 6 Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema? Bwana, utuinulie nuru ya uso wako. 7 Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai. 8 Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.