Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 64.1
Bible en Swahili de l’est


1 Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu; Unilinde uhai wangu na hofu ya adui.Psaumes 27.7 Psaumes 34.4 Lamentations 3.55-3.56 Psaumes 140.1 Psaumes 17.8-17.9
2 Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya, Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;Jérémie 11.19 Psaumes 56.6 Matthieu 26.3-26.4 Psaumes 109.2-109.3 Psaumes 31.20
3 Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,Psaumes 58.7 Psaumes 57.4 Psaumes 11.2 Proverbes 12.18 Jacques 3.6-3.8
4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.Psaumes 55.19 Psaumes 11.2 1 Samuel 18.11 Psaumes 64.7 Psaumes 59.3-59.4
5 Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Husema, Ni nani atakayeiona?Psaumes 10.11 Psaumes 140.5 Psaumes 94.7 1 Samuel 23.19-23.23 Psaumes 59.7
6 Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili; Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao, Na moyo wake, huwa siri kabisa.Psaumes 49.11 Daniel 6.4-6.5 Jean 19.7 1 Samuel 24.9 Esaïe 29.15
7 Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha, Kwa mshale mara watapigwa.Psaumes 7.12-7.13 Lamentations 3.12-3.13 1 Chroniques 10.3-10.7 Deutéronome 32.42 Proverbes 29.1
8 Ndivyo watakavyokwazwa, Ulimi wao wenyewe ukishindana nao. Wote wawaonao watatikisa kichwa.Proverbes 18.7 Proverbes 12.13 Luc 19.22 Jérémie 18.16 Psaumes 22.7
9 Na watu wote wataogopa, Wataitangaza kazi ya Mungu, Na kuyafahamu matendo yake.Jérémie 51.10 Jérémie 50.28 Psaumes 40.3 Esaïe 5.12 Psaumes 107.42-107.43
10 Mwenye haki atamfurahia Bwana na kumkimbilia, Na wote wenye moyo wa adili watajisifu.Job 22.19 Psaumes 25.20 Psaumes 112.2 Psaumes 97.11 Psaumes 11.1

Cette Bible est dans le domaine public.