Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 70
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, uniokoe, Ee Bwana, unisaidie hima. 2 Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu. 3 Warudi nyuma, na iwe aibu yao, Wanaosema, Ewe! Ewe! 4 Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu. 5 Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Bwana, usikawie.

Cette Bible est dans le domaine public.