Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 82 Bible en Swahili de l’est
Condamnation des oppresseurs et de leur injustice
1 Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu. 2 Hata lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya? 3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara; 4 Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu. 5 Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika. 6 Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia. 7 Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu. 8 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe utawarithi mataifa yote.