Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 3.1
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana akaniambia, Enenda tena, mpende mwanamke apendwaye na rafiki yake, naye ni mzinzi; kama vile Bwana awapendavyo wana wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikate ya zabibu kavu.Osée 1.2-1.3 Jérémie 3.12-3.14 Jérémie 3.20 Jérémie 3.1-3.4 Psaumes 123.2
2 Basi nikajinunulia mwanamke huyo kwa vipande kumi na vitano vya fedha, na homeri moja ya shayiri, na nusu ya homeri ya shayiri;Lévitique 27.16 Ezéchiel 45.11 Exode 22.17 1 Samuel 18.25 Esaïe 5.10
3 nami nilimwambia, Utatawa kwa ajili yangu siku nyingi; hutafanya mambo ya ukahaba, wala hutakuwa mke wa mtu awaye yote; nami nitakuwa hali iyo hiyo kwa ajili yako.Deutéronome 21.13
4 Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago;Juges 17.5 Genèse 31.19 Daniel 12.11 Juges 8.27 1 Samuel 23.9
5 baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho.Jérémie 50.4-50.5 Jérémie 30.9 Esaïe 2.2 Ezéchiel 37.22-37.25 Ezéchiel 34.23-34.24

Cette Bible est dans le domaine public.