Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 123 Bible en Swahili de l’est
Prière pour le peuple opprimé
1 Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni. 2 Kama vile macho ya watumishi Kwa mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Kwa mkono wa bibi yake; Hivyo macho yetu humwelekea Bwana, Mungu wetu, Hata atakapoturehemu. 3 Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu sisi, Kwa maana tumeshiba dharau. 4 Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, Na dharau ya wenye kiburi.