Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Job 25 Bible en Swahili de l’est
Intervention n° 3 de Bildad
1 Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema, 2 Enzi na hofu zi pamoja naye; Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka. 3 Je! Majeshi yake yahesabika? Ni nani asiyetokewa na mwanga wake? 4 Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke? 5 Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake; 6 Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!