Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 1
Bible en Swahili de l’est


1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Psaumes 26.4-26.5 Proverbes 4.14-4.15 Jérémie 15.17 Proverbes 13.20 Psaumes 119.1-119.2
2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Josué 1.8 Psaumes 119.35 Psaumes 119.11 Psaumes 119.92 Romains 7.22
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. Jérémie 17.8 Ezéchiel 47.12 Psaumes 92.14 Ezéchiel 19.10 Genèse 39.3
4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Job 21.18 Matthieu 3.12 Esaïe 17.13 Psaumes 35.5 Esaïe 29.5
5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. Psaumes 5.5 Malachie 3.18 Luc 21.36 Matthieu 25.46 Matthieu 25.32
6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. 2 Timothée 2.19 Nahum 1.7 Jean 10.14 Psaumes 37.18-37.24 Psaumes 146.9

Cette Bible est dans le domaine public.