Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 112.10 Bible en Swahili de l’est
1 Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake. 2 Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. 3 Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele. 4 Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. 5 Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki. 6 Kwa maana hataondoshwa kamwe; Mwenye haki atakumbukwa milele. 7 Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana. 8 Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa. 9 Amekirimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.10 Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuyeyuka, Tamaa ya wasio haki itapotea.