Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 112.10
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake.Psaumes 128.1 Psaumes 119.16 Psaumes 111.10 Esaïe 50.10 Romains 8.6
2 Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.Genèse 17.7 Psaumes 102.28 Psaumes 25.13 Proverbes 20.7 Psaumes 37.26
3 Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele.Proverbes 3.16 Proverbes 15.6 Matthieu 6.33 Psaumes 112.9 Psaumes 111.3
4 Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki.Job 11.17 Psaumes 97.11 Jean 12.46 Esaïe 50.10 Luc 6.36
5 Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki.Psaumes 37.25-37.26 Deutéronome 15.7-15.10 Proverbes 12.2 Proverbes 24.27 Psaumes 37.21
6 Kwa maana hataondoshwa kamwe; Mwenye haki atakumbukwa milele.Proverbes 10.7 Psaumes 15.5 Psaumes 55.22 Psaumes 62.6 Hébreux 6.10
7 Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana.Psaumes 57.7 Proverbes 1.33 Esaïe 26.3-26.4 Psaumes 64.10 Psaumes 34.4
8 Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa.Psaumes 59.10 Psaumes 91.8 Psaumes 118.7 Hébreux 13.9 Psaumes 31.24
9 Amekirimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.Psaumes 75.10 Psaumes 92.10 Hébreux 6.10 Hébreux 13.16 1 Jean 3.16-3.18
10 Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuyeyuka, Tamaa ya wasio haki itapotea.Proverbes 11.7 Luc 13.28 Psaumes 37.12 Psaumes 58.7-58.8 Proverbes 10.28

Cette Bible est dans le domaine public.