Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 124.3 Bible en Swahili de l’est
Dieu protège et délivre les siens
1 Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa, 2 Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia. 3 Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu 4 Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu; 5 Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo. 6 Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. 7 Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. 8 Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.