Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 13.6
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, hata lini utanisahau, hata milele? Hata lini utanificha uso wako?Job 13.24 Psaumes 89.46 Psaumes 94.3-94.4 Psaumes 6.3 Psaumes 44.24
2 Hata lini nifanye mashauri nafsini mwangu, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Hata lini adui yangu atukuke juu yangu?Michée 7.8-7.10 Jérémie 15.18 Jérémie 8.18 Ecclésiaste 5.17 Job 10.15
3 Ee Bwana, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.Jérémie 51.39 Esdras 9.8 Psaumes 5.1 Psaumes 18.28 Psaumes 119.153
4 Adui yangu asije akasema, Nimemshinda; Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.Psaumes 25.2 Psaumes 38.16 Jérémie 1.19 Psaumes 112.6 Lamentations 1.16
5 Nami nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.Psaumes 9.14 Psaumes 52.8 Habakuk 3.18 Luc 1.47 1 Samuel 2.1
6 Naam, nimwimbie Bwana, Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.Psaumes 116.7 Psaumes 119.7 Psaumes 21.13

Cette Bible est dans le domaine public.