Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 3.7 Bible en Swahili de l’est
1 Bwana, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia, 2 Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. 3 Na Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. 4 Kwa sauti yangu namwita Bwana Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. 5 Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza. 6 Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote.7 Bwana, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.8 Wokovu una Bwana; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.