Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 4
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Umenifanyizia nafasi wakati wa shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu. Psaumes 18.18-18.19 Psaumes 17.6 Habakuk 3.19 Job 36.16 Jérémie 23.6
2 Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo? Osée 4.7 Psaumes 3.3 Psaumes 5.6 Ephésiens 4.25 1 Samuel 12.21
3 Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa; Bwana atasikia nimwitapo. 2 Pierre 2.9 2 Timothée 2.19 2 Thessaloniciens 2.13-2.14 Psaumes 50.5 Psaumes 6.8
4 Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia. Ephésiens 4.26 Psaumes 77.6 Psaumes 63.6 Psaumes 46.10 2 Corinthiens 13.5
5 Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana. Deutéronome 33.19 Psaumes 37.3 Psaumes 51.19 Psaumes 62.8 Esaïe 50.10
6 Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema? Bwana, utuinulie nuru ya uso wako. Psaumes 80.7 Psaumes 80.19 Nombres 6.26 Psaumes 89.15 Psaumes 67.1
7 Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai. Esaïe 9.3 Psaumes 63.2-63.5 Cantique 1.4 Juges 9.27 Actes 14.17
8 Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama. Psaumes 3.5 Lévitique 25.18-25.19 Deutéronome 12.10 Lévitique 26.5 Psaumes 16.8-16.9

Cette Bible est dans le domaine public.