Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 54.4 Bible en Swahili de l’est
1 Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu. 2 Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu. 3 Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao.4 Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia; Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.5 Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako. 6 Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee Bwana, nitalishukuru jina lako, maana ni jema. 7 Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu.