Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 67.6 Bible en Swahili de l’est
Louange universelle à Dieu
1 Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake. 2 Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote. 3 Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru. 4 Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani. 5 Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru. 6 Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu wetu, ametubariki. 7 Mungu atatubariki sisi; Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.