Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 93.2 Bible en Swahili de l’est
Le règne de Dieu sur l’univers
1 Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike; 2 Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele. 3 Ee Bwana, mito imepaza, Mito imepaza sauti zake, Mito imepaza uvumi wake. 4 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu. 5 Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele.