Bénédiction future d’Israël
1 Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi.
Esaïe 51.3 Esaïe 55.12-55.13 Esaïe 29.17 Esaïe 4.2 Osée 14.5-14.6
2 Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Bwana, ukuu wa Mungu wetu.
Esaïe 60.13 Esaïe 25.9 Esaïe 55.12-55.13 Esaïe 60.1-60.3 Romains 10.15
3 Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea.
Hébreux 12.12 Job 4.3-4.4 Actes 18.23 Job 16.5 Juges 7.11
4 Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi.
Esaïe 34.8 Esaïe 28.16 Esaïe 32.4 Malachie 3.1 Apocalypse 1.7
5 Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa.
Esaïe 42.6-42.7 Esaïe 29.18 Esaïe 32.3-32.4 Esaïe 50.4 Ephésiens 5.14
6 Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani.Luc 11.14 Jean 5.8-5.9 Matthieu 12.22 Matthieu 9.32-9.33 Esaïe 32.4
7 Na mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi.
Esaïe 34.13 Esaïe 13.22 Esaïe 49.10 Esaïe 44.3-44.4 Apocalypse 18.2
8 Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.
Matthieu 7.13-7.14 Hébreux 12.14 Tite 2.11-2.14 1 Pierre 1.14-1.15 Esaïe 42.16
9 Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo.
Esaïe 62.12 1 Pierre 1.18 Psaumes 107.2 Osée 2.18 Lévitique 26.6
10 Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.
Apocalypse 21.4 Esaïe 25.8 Esaïe 65.19 Esaïe 30.19 Apocalypse 18.20