Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 110.4 Bible en Swahili de l’est
Le Messie, roi et prêtre
1 Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako. 2 Bwana atainyosha toka Sayuni Fimbo ya nguvu zako. Uwe na enzi kati ya adui zako; 3 Watu wako wanajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako. 4 Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki. 5 Bwana yu mkono wako wa kuume; Ataseta wafalme, Siku ya ghadhabu yake. 6 Atahukumu kati ya mataifa, Ataijaza nchi mizoga; Ataseta kichwa katika nchi nyingi. 7 Atakunywa maji ya mto njiani; Kwa hiyo atakiinua kichwa chake.