Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 126.2 Bible en Swahili de l’est
1 Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto.2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu.3 Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi. 4 Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini. 5 Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. 6 Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.