Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 128.2 Bible en Swahili de l’est
1 Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake.2 Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.3 Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako. 4 Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana. 5 Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; 6 Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.