Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 137 Bible en Swahili de l’est
Souffrance des exilés
1 Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni. 2 Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu. 3 Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. 4 Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni? 5 Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe, Mkono wangu wa kuume na usahau. 6 Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu. 7 Ee Bwana, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ya Yerusalemu. Waliosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini! 8 Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi. 9 Heri yeye atakayewakamata wadogo wako, Na kuwaseta wao juu ya mwamba.