Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 149.4 Bible en Swahili de l’est
Louange à Dieu pour ses jugements
1 Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa. 2 Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao. 3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie. 4 Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu. 5 Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao. 6 Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao. 7 Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, Na adhabu juu ya kabila za watu. 8 Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, Na wakuu wao kwa pingu za chuma. 9 Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote. Haleluya.