Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 57
Bible en Swahili de l’est


1 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hata misiba hii itakapopita. Psaumes 91.4 Esaïe 26.20 Psaumes 63.7 Psaumes 36.7 Ruth 2.12
2 Nitamwita MUNGU Aliye juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu. Psaumes 138.8 Philippiens 1.6 Esaïe 26.12 Hébreux 13.21 Esaïe 57.15
3 Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa, Atukanapo yule atakaye kunimeza. Mungu atazipeleka Fadhili zake na kweli yake Psaumes 40.11 Psaumes 56.1-56.2 Psaumes 43.3 Nombres 23.24 Actes 12.11
4 Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali. Psaumes 58.6 Psaumes 55.21 Psaumes 64.3 Proverbes 12.18 Psaumes 35.17
5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako. Habakuk 2.14 Esaïe 6.3 Psaumes 72.19 Psaumes 57.11 Nombres 14.21
6 Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nafsi yangu imeinama; Wamechimba shimo mbele yangu; Wametumbukia ndani yake! Psaumes 145.14 Psaumes 140.5 Psaumes 9.15-9.16 Psaumes 142.3 Psaumes 35.7-35.8
7 Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Moyo wangu u thabiti. Nitaimba, nitaimba zaburi, Psaumes 112.7 Romains 5.3 Psaumes 108.1-108.5 Esaïe 24.15 Psaumes 34.4
8 Amka, utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri. Psaumes 16.9 Psaumes 30.12 Juges 5.12 Esaïe 52.9 Psaumes 150.3
9 Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu, Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa. Psaumes 138.1 Psaumes 96.3 Psaumes 18.49 Psaumes 2.1 Psaumes 22.22-22.23
10 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni, Na uaminifu wako hata mawinguni. Psaumes 103.11 Psaumes 36.5 Psaumes 108.4 Esaïe 54.7-54.10 Psaumes 71.19
11 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako. Psaumes 57.5 Psaumes 8.9 Apocalypse 15.3-15.4 Psaumes 8.1

Cette Bible est dans le domaine public.