Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 6
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako. Psaumes 38.1 1 Chroniques 15.21 Jérémie 46.28 Jérémie 10.24 Esaïe 54.9
2 Bwana, unifadhili, maana ninanyauka; Bwana, uniponye, mifupa yangu imefadhaika. Osée 6.1 Nombres 12.13 Psaumes 31.10 Psaumes 30.2 Job 19.21
3 Na nafsi yangu imefadhaika sana; Na Wewe, Bwana, hata lini? Psaumes 90.13 Jean 12.27 Psaumes 38.8 Psaumes 22.14 Psaumes 77.7
4 Bwana urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. Psaumes 17.13 Psaumes 22.20 Psaumes 116.4 Psaumes 80.14 Psaumes 90.13
5 Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru? Ecclésiaste 9.10 Psaumes 88.10-88.12 Psaumes 30.9 Psaumes 115.17 Psaumes 118.17
6 Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu. Psaumes 69.3 Psaumes 42.3 Psaumes 38.9 Job 7.3 Psaumes 39.12
7 Jicho langu limeharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi. Psaumes 38.10 Job 17.7 Psaumes 88.9 Lamentations 5.17 Psaumes 32.3
8 Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa Bwana ameisikia sauti ya kilio changu. Luc 13.27 Psaumes 119.115 Psaumes 3.4 Matthieu 7.23 Psaumes 139.19
9 Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu. Psaumes 66.19-66.20 Psaumes 116.1-116.2 Psaumes 120.1 Jonas 2.2 Psaumes 3.4
10 Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika. Jérémie 20.11 Psaumes 86.17 Psaumes 132.18 Malachie 3.18 Psaumes 7.6

Cette Bible est dans le domaine public.