Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 98.3 Bible en Swahili de l’est
Louange universelle au juste Juge
1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. 2 Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. 3 Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. 4 Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. 5 Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. 6 Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana. 7 Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. 8 Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha. 9 Mbele za Bwana; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili.