Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 12
Bible en Swahili de l’est


1 Na katika siku hiyo utasema, Ee Bwana, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo. Esaïe 25.1 Psaumes 30.5 Esaïe 54.8 Esaïe 40.1-40.2 Esaïe 66.13
2 Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Exode 15.2 Psaumes 118.14 Psaumes 27.1 Esaïe 45.22-45.25 Apocalypse 7.10
3 Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. Apocalypse 22.17 Jérémie 2.13 Apocalypse 22.1 Esaïe 55.1-55.3 Esaïe 49.10
4 Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litajeni jina lake kuwa limetukuka. Psaumes 105.1 Psaumes 18.46 Psaumes 117.1-117.2 Psaumes 145.4-145.6 Exode 33.19
5 Mwimbieni Bwana; kwa kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya katika dunia yote. Exode 15.1 Psaumes 98.1 Psaumes 105.2 Exode 15.21 Psaumes 72.19
6 Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako. Zacharie 2.10-2.11 Sophonie 3.14-3.17 Zacharie 2.5 Esaïe 41.16 Psaumes 9.11

Cette Bible est dans le domaine public.