1 Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
Genèse 30.23 Esaïe 13.12 Esaïe 2.17 Esaïe 3.25-3.26 Luc 1.25
Purification et gloire d’Israël
2 Siku hiyo chipukizi la Bwana litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.
Zacharie 6.12 Zacharie 3.8 Jérémie 23.5 Joël 2.32 Jérémie 33.15
3 Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu;
Luc 10.20 Esaïe 52.1 Esaïe 60.21 Colossiens 3.12 Romains 11.5
4 hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza.
Ezéchiel 36.25 Malachie 3.2-3.3 Zacharie 13.1 Ezéchiel 22.15 Zacharie 13.9
5 Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara.Exode 13.21-13.22 Nombres 9.15-9.22 Esaïe 46.13 Esaïe 33.20 Exode 40.34-40.38
6 Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.
Esaïe 25.4 Psaumes 27.5 Esaïe 32.2 Psaumes 91.1 Proverbes 18.10